Leseni Halali ya TAVIC

TAVIC inalinda na kusimamia haki za wabunifu na wamiliki wa kazi za sauti na taswira kwa kuhakikisha matumizi ya kazi zao yanatambuliwa na mirahaba inayostahili inakusanywa na kugawanywa kwa haki.

TAKWA LA KISHERIA & FAIDA

Kwa Nini Biashara Yako Inahitaji Leseni ya TAVIC?

Kucheza au kuonyesha kazi za sauti na picha hadharani bila leseni ni kosa la kisheria. Pata leseni ufaidi amani na heshima ya kibiashara.

Omba Leseni

Uhalali Kisheria Chini ya Cap 218

Inalinda biashara yako dhidi ya ukaguzi, faini za kisheria, na migogoro ya hati miliki kwa kufuata Sheria Sura ya 218 R.E. 2002.

Malipo Salama kwa Control Number

Unapokea Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number) na kulipia kwa njia rasmi za kibenki au Mobile Money (M-Pesa/NMB/CRDB).

Cheti & Beji ya Heshima 2026

Baada ya malipo, unapokea Cheti Halali cha Leseni cha kuonyeshwa katika eneo la mapokezi la biashara yako kusaidia uchumi wa sanaa.

Amani ya Kibiashara na Wateja

Wateja wako wanastahimili burudani ya filamu na muziki bila wasiwasi au usumbufu wowote wa kisheria au ukaguzi wa ghafla.

Restaurant and Bar with TV screens

Maeneo ya Hadhara & Burudani

Hoteli, Baa, Migahawa na Kumbi zinazocheza maudhui ya TV/Muziki hadharani.

MAKUNDI YA WATUMIAJI

Nani Anapaswa Kupata Leseni ya TAVIC?

Hoteli & Migahawa

Vyumba & Mapokezi

Baa & Vilabu

Lounge & Nightclubs

TV & Redio

Vituo vya Utangazaji

Kumbi za Sherehe

Harusi & Matamasha

Usafiri wa Umma

Mabasi ya Filamu

Majukwaa Online

Apps & Streaming

HATUA RAHISI 4

Mchakato wa Kupata Leseni Halali ya TAVIC

Pata leseni yako kwa sekunde chache kupitia mfumo wetu wa kidijitali wa Control Number.

1

Jaza Fomu ya Maombi

Jaza fomu mtandaoni au pakua fomu ya PDF na kututumia.

2

Pokea Control Number

TAVIC itakukotolewa ada na kukutumia Control Number ya Malipo.

3

Lipa kwa Benki/Simu

Lipa ada kupitia M-Pesa, Tigo Pesa, NMB, CRDB Bank au AZANIA Bank.

4

Pokea Cheti Rasmi

Pokea Cheti Halali cha Leseni cha kuonyeshwa katika eneo lako la biashara.

ELIMU NA UWAJIBIKAJI

Warsha na Semina za Hakimiliki kwa Wasanii Tanzania

TAVIC inaandaa semina, warsha, na programu za mafunzo maalum katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania ili kuwaelimisha wazalishaji, wakurugenzi, na waigizaji kuhusu Sheria ya Hakimiliki Sura ya 218 na jinsi ya kulinda maslahi ya kazi zao.

50+ Warsha Zilizofanyika
10,000+ Wasanii Walioelimishwa
Conference Seminar
Maswali ya Mara kwa Mara

Kwa Nini Uwasiliane Nasi?

Majibu ya kina kwa maswali ya kisheria, utoaji wa leseni, uanachama, na mirabaha chini ya Kanuni za Hakimiliki.

Je, TAVIC ni nini?

Tanzania Audiovisual Collection Limited (TAVIC) ni Taasisi ya Usimamizi wa Pamoja wa Hakimiliki (CMO) iliyopewa mamlaka kisheria na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kusimamia haki za kiuchumi kwa pamoja kwa waundaji wa sauti na picha.

Usimamizi wa Pamoja ni Nini?

Usimamizi wa pamoja ni mfumo ambapo wasanii wanaiwezesha taasisi moja (TAVIC) kukusanya ada za mirabaha na kulinda haki zao kwa pamoja badala ya kila msanii kufanya hivyo binafsi.

Kwa nini TAVIC ilianzishwa?

Ilianzishwa ili kutoa suluhisho la kudumu la kulinda na kuratibu mirabaha ya wasanii wa kazi za audiovisual Tanzania.

Nani anahitaji leseni kutoka TAVIC?

Wamiliki wote wa biashara wanaocheza au kuonyesha kazi za audiovisual hadharani, ikiwa ni pamoja na baa, hoteli, vyombo vya habari (TV na Redio), na kumbi za starehe.

Je, mirabaha inakusanywaje na kugawanywaje?

Ada za leseni hukusanywa kutoka kwa watumiaji na kugawanywa kwa wanachama kulingana na data ya matumizi ya kazi zao na kulingana na mwongozo rasmi wa usambazaji.

TAVIC inapatikana wapi?

Ofisi zetu kuu zinapatikana Dar es Salaam, na unaweza pia kuwasiliana nasi mtandaoni kupitia tovuti rasmi au mitandao ya kijamii.

TAVIC Team

Uzingatiaji Kamili wa Kisheria 100%

Imeidhinishwa na Kukaguliwa PCMO na COSOTA