TAVIC ni chombo cha usimamizi wa pamoja wa hakimiliki (Collective management organization) kinachowawakilisha wzalishaji, wakurugenzi, waigizaji na wataalam wote wa sekta ya sauti na picha nchini Tanzania chini ya sheria ya hakimiliki sura ya 218 R.E 2002 .
Kuimarisha maslahi ya kiuchumi ya wazalishaji na waigizaji wa Tanzania.
Sekta ya sauti na picha (audiovisual) ya Tanzania inayostawi, ambapo ubunifu unalindwa, unathaminiwa kisheria, na kutuzwa kupitia mirabaha yenye haki.
Kusimamia na kulinda kwa pamoja haki za kiuchumi za wabunifu wa kazi za sauti na picha kupitia ukusanyaji wa mirabaha wenye uwazi, mgawanyo wa haki, kutoa elimu ya hakimiliki, na kukuza ushirikiano wa kisekta.
TAVIC inaandaa semina, warsha, na programu za mafunzo maalum katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania ili kuwaelimisha wazalishaji, wakurugenzi, na waigizaji kuhusu Sheria ya Hakimiliki Sura ya 218 na jinsi ya kulinda maslahi ya kazi zao.
Tunatoa huduma kamili za kisheria na usimamizi wa kiuchumi ili kutoa thamani halisi ya kazi za audiovisual.
Kusajili rasmi wazalishaji, waigizaji, wakurugenzi na kukusanya daftari la kazi zote za audiovisual nchini.
Kukusanya ada za ushuru wa matumizi na kuzigawa kwa wanachama kulingana na ripoti za matumizi (broadcast logs).
Kuandaa warsha, semina, na kutoa elimu kwa umma na vyombo vya habari kuhusu sheria za haki miliki.
Kutoa msaada wa kisheria dhidi ya matumizi haramu na wizi wa kazi za sanaa (piracy) chini ya Sura ya 218.
Kutoa leseni za matumizi kwa vituo vya TV/redio, hoteli, baa, na majukwaa ya mtandaoni yanayocheza kazi za audiovisual.
Majibu ya kina kwa maswali ya kisheria, utoaji wa leseni, uanachama, na mirabaha chini ya Kanuni za Hakimiliki.
Tanzania Audiovisual Collection Limited (TAVIC) ni Taasisi ya Usimamizi wa Pamoja wa Hakimiliki (CMO) iliyopewa mamlaka kisheria na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kusimamia haki za kiuchumi kwa pamoja kwa waundaji wa sauti na picha.
Usimamizi wa pamoja ni mfumo ambapo wasanii wanaiwezesha taasisi moja (TAVIC) kukusanya ada za mirabaha na kulinda haki zao kwa pamoja badala ya kila msanii kufanya hivyo binafsi.
Ilianzishwa ili kutoa suluhisho la kudumu la kulinda na kuratibu mirabaha ya wasanii wa kazi za audiovisual Tanzania.
Wamiliki wote wa biashara wanaocheza au kuonyesha kazi za audiovisual hadharani, ikiwa ni pamoja na baa, hoteli, vyombo vya habari (TV na Redio), na kumbi za starehe.
Ada za leseni hukusanywa kutoka kwa watumiaji na kugawanywa kwa wanachama kulingana na data ya matumizi ya kazi zao na kulingana na mwongozo rasmi wa usambazaji.
Ofisi zetu kuu zinapatikana Dar es Salaam, na unaweza pia kuwasiliana nasi mtandaoni kupitia tovuti rasmi au mitandao ya kijamii.
Imeidhinishwa na Kukaguliwa CMO na COSOTA